Friday, July 10, 2009

MKE KUMZIDI MUME KIPATO NI TATIZO?


Ikiwa kama ijumaa ningependa kuanza kwa kuuliza swali hili; Ikiwa mkeo ana kazi nzuri zaidi yako na kipato chake ni kikubwa zaidi yako, je hili lina uhusiano wowote na matatizo kwenye ndoa?

Nina ndugu ambaye kwa mtizamo wake anasema ikiwa mke kakuzidi kipato sikuzote atataka kumyanyasa mume wake.. Bahati mbaya au nzuri pia kapata mchumba mwenye kipato juu yake. Sasa yuko njia panda hajui afanye nini na kumpenda ana mpenda...

Wadau ushauri unahitajika..

1 comment:

  1. ushauri wangu kama kampenda asiogope kipato chake au kazi yake anachopaswa kujua huyo dada naye anampenda au la na kama anampenda hawezi kumnyanyasa kwani mtu unayempenda huwezi kumkosesha amani huu ndio mtazamo wangu
    shany

    ReplyDelete