Wednesday, July 1, 2009

Msaada wa malavidavi

Habari dada,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 40, na nilikuwa nimeoa kwa miaka 10 ila sikubahatika kupata mtoto, na ndoa yangu haikudumu na ikapelekea mimi kuachana na mke wangu. Sababu kubwa ni kwamba nilimfumania mke wangu na mwanaume mwingine hotelini wakiwa katika shughuli za kimahaba. Roho iliniuma sana na ikapelekea mimi kumfukuza mke wangu na kuachana nae. Kwa sasa nina mwaka mmoja tangu tuachane,ila kuna wakati huwa namkumbuka sana mke wangu.
Hivi majuzi mke wangu kanipigia akiniomba msamaha na kwamba angependa kurudi kwangu tuishi pamoja maana bado ananipenda. Dada mimi niko njia panda maana sielewi nimjibu nini kwa kipindi hiki, je nimruhusu arudi au nimkatalie? Tafadhali naomba wadau wanishauri maana niko njia panda. Kumpenda bado nampenda ila sijasahau alivyonitenda...
Tafadhali wekajina langu kapuni..
Asante sana dada....

1 comment:

  1. pole kwa mkasa uliokukuta. Nakushauri kama bado unampendana msamehe na mrudie tu mkeo kwa sababu binadamu hukosa na km amegundua makosa yake basi huna budi kumsamehe.

    ReplyDelete