Tuesday, June 23, 2009

MAJISIFU BAADA YA NGONO


Wasalaam wapenzi wa kablog ketu ka malavidavi na pesa.

Kuna suala zima limekuwa likinitatiza sana mara kwa mara ninapokuwa vijiweni au kwenye mijumuiko ya kijamii, na suala hili ni majisifu baada ya mtu kufanya mapenzi/ngono na mwenzie. Utakuta kijana anajisifia kwa wenzake, eti mimi yule demu nshamkaza sana au nshazini nae sana tu. Mtu huyu anachukulia kama vile kitendo hicho ni cha ufahari sana mbele za watu. Maswali ninayojiuliza mpaka leo sipati majibu ni; Hivi kutenda ngono na mtu ni sifa? Na kama mlikuwa wawili wakati wa ngono, jamii inahusika vipi na habari hii? Au nia huwa ni kumchafulia tabia mwenzako na kumdhalilisha?

Binafsi sioni cha ajabu sana kuhusiana na hili, maana ni maamuzi yenu wenyewe, tena mtu mwingine utakuta anamuongelea mke mtarajiwa wake namna hiyo. Sasa hii ni sifa au ulimbukeni????

Wadau yangu ni hayo tu kutoka mtaani kwetu. Karibuni kwa mchango wa mawazo.

2 comments:

  1. sure hapo umesema manake aka katabia wanaume wanakapenda kweli

    ReplyDelete
  2. NI UJINGA NA ULIMBUKENI. HUENDA HILO LIJAMAA LINALOONGEA HIVYO, HALIJAPATA KITU KAZI KUJISIFU TU. DAWA YAKE NI KUMSHUSHUA HAPO HAPO, ATAJIONA MDOGO KAMA PIRITON.

    ReplyDelete